You are currently viewing Tahadhari!!!Dola inataka kufanya uharamia dhidi ya wapigakura jimbo la Mtambwe!

Tahadhari!!!Dola inataka kufanya uharamia dhidi ya wapigakura jimbo la Mtambwe!

Mgombea wa ACT Wazalendo Jimbo la Mtambwe ameenguliwa ugombea kwa kisingizio cha kuwa na vitambulisho viwili vya Mzanzibari mkaazi. Huu ni uhuni wa serikali ya Mwinyi kuhadaa CCM wenzake kwamba anakubalika na upinzani hauna vigenzo Zanzibar! Uhalisia wa jambo hili uko hivi —— kitambulisho cha pili cha mgombea wa ACT kimetengenezwa wiki hii na kukamilika jana usiku wa manane chini ya usimamizi wa Msimamizi wa Uchaguzi Wilaya ya Wete m Issa Juma na Msimamizi wa Vitambulisho Wilaya ya Wete Bakari Hamad Issa. Hawa ni vinara wa ubakaji huu wa demokrasia na haki ya watu wa Mtambwe! Inshallah watajibu dhulma hii!

Kitambulisho hicho walichotengeneza mpaka dakika hii katika mfumo wa Vitambulisho kinasoma NotAlive na bado hawajaprint.Taarifa za siri zinasema tayari msimamizi wa vitambulisho Wilaya ya Wete, ameshakituma kitambulisho hicho katika system kwa ajili ya kuwekwa alive na kuprintiwa Unguja na leo hii kitaprintiwa.Kitambulisho chake halali ni hiki hapa!

Baada ya kuprintiwa kitambulisho pamoja na Barua ya Bwana Bakari vitatumika kama ushahidi katika rufaa ya kutoteuliwa kwa mgombea wa ACT hivyo mgombea kutupiliwa mbali pingamizi lake.ACT Wazalendo chukueni hatua kwenye jambo hili haraka!Mwinyi amefanya ufisadi wa kihistoria Zanzibar na kuna uwezekano mkubwa system isimrudishe.! Hii michezo ni ya 2025 kujaribu kuonesha ana pumzi Zanzibar!

Shirikisha