You are currently viewing Ufisadi Zanzibar: Kazi ya kuiua PBZ inaendelea

Ufisadi Zanzibar: Kazi ya kuiua PBZ inaendelea

Waasisi wa mapinduzi walikuwa na ndoto ya mfumo wa kifedha unaompa ahueni na uhuru Mzanzibari. 1966 ndoto yao ikaleta PBZ. Miaka zaidi ya hamsinini PBZ imefanya kazi yake leo kaja mtu kaamua ife kwa hila. Wajua anaifanyia hujuma gani? Anainyima uwezo kufanya biashara! Rais huyu anayajuwa mapinduzi na lengo lake?

Habari sasa ishasambaa kuwa kaamuwa skuli zote za sekondari Unguja na Pemba zaidi ya skuli 250 zifungulishwe akaunti za NMB na sio PBZ!! Benki yetu fahari na utambulisho wa Zanzibar inaingia mwambani! CCM tushafahamu mnasubiri 2025 kumwondoa huyu bwana lakini tunawakumbusha hayupo alowahi kuidhulumu Zanzibar akaishi kwa raha hadi umauti!

Shirikisha