Kuna mjadala mkubwa unaendelea kuhusu Uchaguzi Mkuu Zanzibar 2025. Wahafidhina wa CCM Zanzibar inasemekana wameamua Hussein Mwinyi asirudi kugombea kama ilivyo utamaduni wa CCM wa vipindi viwili. Hawa wanaungwa mkono na Wazanzibari wanaopinga ufisadi wa Mwinyi unaozidi kuibuka siku hadi siku.Wanakabiliana na kundi linalomtetea Mwinyi ambalo kwa kiasi kikubwa ndilo linalotajwa kumzamisha kimaadili. Kama hili litafanikiwa itakuwa si mara ya kwanza Zanzibar kuwa na Rais wa muhula mmoja.
Baadhi ya mambo ambayo yako kwenye faili maalum la siri la tathmini ya Urais wa Mwinyi ni umiliki wa mahoteli mawili ya kitalii kutokana na rushwa kubwa yeye na kikundi chake, uporaji ardhi na kujimilikisha ardhi ya umma katika baadhi ya maeneo Zanzibar, kujimilikisha 30% ya bandari Zanzibar yeye na swahiba wake Toufiq Turky wakiwa na Wafaransa kampuni ya Bollore pamoja na kujitwalia hisa katika kampuni inayoendesha huduma za uwanja wa ndege Zanzibar! Watu wa karibu na Mwinyi wanasema hivi sasa anaishi kama kawehuku na kufanya kila njia kuiba na kujilimbikizia kutokana na kukosa uhakika wa kurudi 2025! “Ameamua liwalo la liwe. Ajikusanyie cha muda mrefu kama baba yake mzee Mwinyi alivyouza Loliondo kwa Waarabu mwaka 1992” kinasema chanzo hicho.!
Mifumo ya siri serikalini na wazee wa CCM tayari wanaifanyia kazi orodha ya majina manne ya watu walio chini ya uangalizi kuchukua nafasi ya Hussein Mwinyi 2025.