You are currently viewing Uchumi wa Zanzibar umekosa dira?

Uchumi wa Zanzibar umekosa dira?

Muheshimiwa Hussein Mwinyi umekopa dola milioni 500 kutoka kwenye benki ya biashara ambayo mkopo wake una riba kubwa sana. Baadhi ya pesa hizi bilioni sitini TZ sh. Umejenga uwanja wa Amaan, uwanja ambao haitumiki kwa mashindano yoyote makubwa na katika mashindano ambayo yanatumika katika kiwanja hicho pesa inayoingia ni chache sana pesa ambayo haiwezi ikarudisha bilioni 60.

Hujatuambia kwamba pesa hizi dola milioni 500 utazilipa vipi? Au hujui kwamba utaondoka madarakani na kutuwachia deni ambalo sisi wananchi ndio itabidi tulilipe kwa kutuzidishia kodi.?

Mheshimiwa Rais, serikali yako imekosa mwelekeo na dira katika mambo muhimu ya jamii.

Umeuza skuli tatu kwa kujenga vibanda vya kuuuza njugu. Umeuza skuli ya darajani, vikokotoni na Tumekuja. Na mbaya kuliko yote umeziuza hizi shule bila ya kujenga nyengine kwenye sehemu husika. Vijana umewapuuza huna hata moja ulolifanya kuzingatia vijana.

Sasa hivi unatuletea story za kujenga taxi za majini wakati hata taxi za mitaani zinatushinda. Majia yote mabovu, traffic lights hazifanyi kazi. Boda boda kila sehemu, nidhamu haipo barabarani, askari wako kila wakikusimamisha wanataka rushwa, kila ofisi mpaka spitali basi lazima utoe hongo ndio upate huduma.

Hivi kweli nyinyi na akili zenu mmkwenda kutumia bilioni 60.kwa kujenga kiwanda cha Amaan ambacho mmengeza seats 3000 just kwa sababu mapinduzi yemefikia miaka 60.

Tumechoka kudanganywa na kupigwa changa la macho na siasa zenu ambazo hazina mwelekeo

Mwananchi wako Mtoni Unguja

Shirikisha